Alhamisi, 21 Agosti 2014

RASIMU YA KATIBA


1.0  JINA NA ANUANI YA KIKUNDI

  • Jina la kikundi litaitwa DUSESCO FAMILY
  • Anuani ya kikundi ni S.L.P ……..
  • Simu no…………..
  • Barua pepe vinyemba@hotmail.com
  • Tarehe ya kuanzishwa ni ……  mwezi ………… mwaka  2014
  • Idadi ya wnachama waanzilishi ilikuwa 17
  • Fungamanisho (Common Bond) ni wakazi wa popote duniani ila tu awe aliyesoma au kufanya akazi Shule ya Sekondari Dumila

 

1.1. MADHUMUNI YA KIKUNDI

Madhumuni ya kikundi hiki ni

  1. kusaidiana katika shida na raha
  2. Kudumisha uhusiano mzuri wa kindugu, kijamaa na kirafiki baina ya wanachama
  3. kupata mahali pa kuhifadhi pesa za wanachama kwa matumizi ya baadae yaliyokusudiwa
  4. kupata mikopo yenye masharti nafuu ya kuendeshea biashara na kuhudumia familia
  5. kujenga utamaduni wa kutoa misaada, michango, kujituma na kujitoa kwaajili ya ndugu zako wa dusesco na jamii kwa ujumla
  6. kuanzisha, kuhimiza na kuendeleza huduma za kijamii kwa lengo la kendeleza    wanachama na jamii kwa ujumla
  7. kushirikiana na wahisan mbali mbali katika kuendeleza na kuboresha  maslahi ya wanachama na wanajamii
  8. kuanzisha na kusimamia mifuko mbalimbali ya maslah ya kundi na wanachama
  9. kutoa elimu mbali mbali kwa malengo ya kutunza na kulinda nidham kwa vijana na wanachama kwa ujumla
  10. kuandaa na kusimamia maendeleo ya taaluma kwa wanakikundi na tegemezi wao

 

1.2. MATARAJIO YA KIKUNDI ILI KUFIKIA MALENGO

  1. wanachama kulipa ada ya kiingilio na ada ya kila mwezi
  2. kuanzisha na kuendeleza shugghuli yeyote ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya wanachama kama  itakavyokubaliwa na wanachama wote wa kikundi.
  3. Kujenga tabia ya kuweka akiba ndani ya kikundi kwa njia ya kulipa ada ya mwezi
  4. Kujenga misingi imara ya kudhibiti ubaguzi, baina ya wanachama pia kudhibiti  ubadhilifu na wizi wa mali za chama
  5. Kujenga umoja ulio imara wenye mshikamano wa kudumu

 

1.3. MAMLAKA YA KIKUNDI NA WAJIBU WAKE

i.                    kupokea wanachama wapya na kuwasajili katika chama kwa kuzingatia sifa za uanachama

 

ii.                  kufanya kazi na kuchukua hatua hatua yoyote kwa makusudi ya kutimiza madhumuni yaliyotajwa katika katiba hii

 

iii.                kuweka mazingira bora kwa wanachama ya kulipa ada za mwezi na kiingilio, faini na michango hiyari.

 

iv.                Kulinda maslahi ya mwanachama

 

v.                  kutafuta wanachama wapya kwa kushirikiana na wanachama wengine

 

vi.                kutatua migogoro baina ya wanachama ili kulinda amani na upendo katika kikundi.

 

vii.              Kutoa adhabu kwa wanachama wake wakorofi kulingana na taratibu zilizokubalika ndani ya kikundi.

 

viii.            Kuunda kamati mbali mbali za uendeshaji katika kikundi

 

 

 

2.0. UANACHAMA

Ili uwe mwanachama wa kikundi cha DUSESCO FAMILY ninlazima uwe na sifa zifuatazo

i.                    mwanachama ni lazima awe amesoma au kufanya kazi katika Shule ya sekondari ya Dumila

ii.                  awe amejiunga na chama hiki na kusajiliwa

iii.                awe amelipa ada ya kiingilio na ada ya kila mwezi na michango yote iliyokubalika katika kikundi

 

2.1. SIFA ZA MWANACHAMA

i.                    awe mwenye umri usiopungua miaka kumi na nane

ii.                  awe ni mwenye akili timamu, tabia nzuri na mwaminifu

iii.                awe tayari kufuata sheria na taratibu za kikundi

ii.                  wanachama watafuata bila kuvunja masharti na kanuni za kuwa wanachama wa DUSESCO FAMILY.

iii.                kila mwanachama anawajibu wa kutumia elimu, fani na nguvu aliyonayo kuwezesha kufikia malengo yaliyoazimiwa.

iv.                Kila mwanachama ni lazima awe amekubali kujiunga kwa hiari yake pasipo kulazimishwa.

v.                  Kila mwanachama ni lazima awe amelipa ada na michango yote iliyokubalika na kikundi

 

2.2. TARATIBU ZA KUJIUNGA KATIKA KIKUNDI

·         Mwombaji atume barua ya maombi ya kujiunga na kikundi kwa Mwenyekiti wa kikundi, na Mwenyekiti atawailisha kwa wanachama wa kikundi ili ajadiliwe. Akikubaliwa maombi yake mwombaji atajibiwa kwa barua au kwa ujumbe kupitia simu na kuelezwa taratibu anazotakiwa kuzifuata ili awe mwanachama kamili.

·         Atasajiliwa katika daftari la kikundi na kutunziwa taarifa zake

·         Kwa mwanachama atakayejiunga kuanzia tarehe 01/01/2015 na kuendelea atalazimika kulipa ada ya kiingilio ambayo ni TSh. 50,000/= (Elfu Hamsini) na ada ya miezi ita iliyopita kwa kiwango atakacho kikuta kipindi husika.

 

 

2.3. WAJIBU WA MWANACHAMA

i.                    kulipa ada ya kiingilio, ada ya mwezi pamoja na michango yote iliyokubaliwa na wanakikundi

ii.                  kuwa mwaminifu ndani na nje ya kikundi

iii.                kutoa taarifa kwenye uongozi wa kikundi au mkutano mkuu wa kikundi iwapo kiongozi anatoa huduma kwa upendeleo au anafanya jambo lolote linalohatarisha maslahi ya kikundi

iv.                kuhudhuria vikao vyote vya kikundi vinavyo muhusu.

v.                  Kuhudhuria sherehe na misiba ya wanachama wenzie

vi.                Kuzingatia sheria za kikundi kikamilifu ikiwemo kulipa faini zote zilizokubalika katika kikundi bila kuonesha ubishi au dharau kwa uongozi au kwa wanachama husika kwa  madhumuni ya kujenga

vii.              Kujielimisha na kuelimisha wengine kuhusu shughuli za kikundi

viii.            Kutumia taaluma uliyo nayo kuelimisha wanachama ili kukuza ufahamu zaidi kwa maslahi ya kikundi

ix.                Kununua hisa na kuweka akiba kwa lengo la kutunisha mfuko

x.                  Kulipa madeni yote kikamilifu kwa muda uliopangwa

xi.                Kuheshimu mikataba ikiwa ni pamoja na kulipa mkopo alioudhamini endapo mkopaji atashindwa kulipa mkopo wake kama alivyoahidi bila sabau za msingi. ( kuheshimu mkataba ni kukubali kuuza dhamana alizoweka ili kufidia deni analodaiwa ndani ya kikundi)

xii.              Kubeba dhamana iwapo janga litatokea dhidi ya hisa za wanachama

 

 

 

2.4. HAKI ZA MWANACHAMA

Kila mwana dusesco anazo haki stahiki zifuatazo

a.       kushiriki shughuli zote za kikundi kwa kufuata kanuni na taratibu za kikundi

    1. kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya kikundi
    2. kuchagua au kuchaguliwa
    3. kuijua katiba ya chama na kuwa nayo pia
    4. kubadili majina ya tegemezi wake tisa
    5. kila mwanakikundi ana haki ya kuheshimiwa na kujaaliwa.
    6. kila mwanachama anayohaki ya kuchangiwa katika nyanja zhifatao

·         ndoa, harusi, send off na kitchen part na beg party

·         uzazi, kuugua na kuuguliwa na mume/mke, watoto 3, baba na mama mzazi

·         kusomesha tegemezi wasiozidi watatu

    1. mwanachama anayohaki ya kumtania mwanachama mwenzie pasipo kumdhahilisha katika group chart ya Dusesco forum
    2. mwanakikundi anayohaki ya kukataa utani katika group chart anaoona kuwa ni wa kumdhalilisha.
    3. kukopeshwa fedha au chombo chochote anachohitaji kwa malengo ya kujiendeleza kiuchumi, ikiwa tu ni mwanachama hai na ametimiza vigezo vyote vya kukopeshwa.
    4. Kusaidiwa gharama za kusafirisha msiba wa tegemezi wake watano na kupewa rambi rambi
    5. Kusimia shughuli za mazishi ya mwanachama mwenyewe kwa ailimia mia moja. Hii ni kusafirisha mwili wake mpaka kwao. Na kulipia gharama zote za mazishi na si vinginevyo.
    6. Kuitikiwa mwaliko alioutoa kwa wanachama wenzie
    7. mwanachama anayohaki ya kushitaki ktk kamati ya nidhamu itakayoundwa na uongozi kwa dhidi ya mwanachama mwenzie aliyemkosea. Aidha anayohaki ya kuomba usuluhisho baina yake na uongozi au mwanachama mwenzie

 

 

 

2.5 KUSIMAMISHWA UANACHAMA

Mwanachama atasimamishwa uanachama wake iwapo atabainika na haya yafuatayo

  • utovu wa nidhamu
  • kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila sababu
  • kutohudhuria shughuli za kikundi hasa katika misiba, sherehe na kutembelea wagonjwa pasipo na sababu za msingi
  • kufanya kitendo chochote ambacho kikundi kitaridhika kuwa ni kitendo cha kutokuwa mwaminifu na kinyume na maadili ya kikundi. Mwanachama huyu atatozwa faini ya shilingi elfu tano (5,000/=) na mara ya pili atafukuzwa uanachama na 15% ya fedha zake zitakatwa kwaajili ya usumbufu.

 

2.6 KUKOMA UANACHAMA

Mwanachama atakuwa amejitoa katika au kutolewa katika kikundi iwapo atakuwa na moja kati ya sifa hizi

i.                    kufariki dunia

ii.                  kuandika barua ya kujitoa katika kikundi na atapewa mafao yake ndani ya siku tisini

iii.                kuukana uanachama kwa hiyari yake

iv.                kufukuzwa uanachama kwa kupigiwa kura isiyopungua theluti mbili ya wanachama waliohudhuria na hii na baada ya kupewa nafasi ya kujitetea kutokana na makosa aliyoyafanya.

v.                  Kutohudhuira vikao vine mfululizo bila ya taarifa maalum

vi.                Kushindwa kulipa ada ya kiingilio mpaka muda wa ziada kupita

vii.              Kushindwa kulipa ada ya mwezi kwa miezi mnne mfululizo

viii.            Kuchukua hisa zake zote katika kikundi

ix.                Ugonjwa wa akili uliothibitioshwa na tabibu.

x.                  Kuhama group

 

3.0 HESABU ZA KIKUNDI

-          Mwaka wa fedha wa kikundi utaanza tarehe …… mwezi .. hadi kila mwaka

-          Kikundi kitaandaa vitabu vya hesabu na kutunza kumbukumbu muhimu

-          Muhtasari wa mahesabu ya fedhu za kikundi utatolewa kila mwezi

-          Muhtasari wa mahesabu ya fedha za kikundi utatolewa na mtunza hazina wa kikundi au yeyote aliyeteuliwa kwa niaba yake.

 

4.0 MUUNDO WA KIKUNDI CHA DUSESCO FAMILY

 

4.1 VIKAO VYA DUSESCO FAMILY

·         kutakuwa na mkutano mkuu mara moja kwa mwaka. Aidha mikutano ya  dharura inaweza kufanyika wakati wowote kwa idhini ya uongozi. Kila mkutano mkuu utawahusisha wanachama, wajumbe wa kamati ya utendaji na wadhamini.

·         mkutano mkuu wa DUSESCO FAMILY utakuwa na mamlaka na madaraka yafuatayo

i.                    kuchagua uongozi mpya

ii.                  kuchagua wadhamini

iii.                kuweka na kuidhinisha kanuni za fedha za utawala

iv.                kuteua viongozi watatu wenye mamlaka ya kuidhinisha hundi au malipo taslim.

v.                  Kupokea na kuzingatia shughuli za wanakikundi

vi.                kupokea na kutathmini taarifa ya maendeleo ya utendaji na kisha kutoa maagizo au nasaha zinazostahili.

vii.              kupokea na kuzingatia taarifa za mapato na matumizi ya kikundi

viii.            kudhibiti au kukataa uamuzi wowote uliotolewa usio na maslahi kwa kikundi kwa wanachama kupiga kura ambayo itaungwa mkono na zaidi ya nusu ya wanakikundi

ix.                kumuondoa kiongozi kwa kupoteza sifa za uongozi au kukiuka masharti ya katiba baada ya kutosheka na ushahidi au sababu za kuchukua hatua hiyo.

x.                  Wanachama wote wa DUSESCO FAMILY watakuwa ndio walinzi wakubwa wa katiba kupitia vikao mbalimbali ambavyo vimeundwa na katiba hii.

xi.                Kushughulikia matatizo yote ya kinidhamu

xii.              Kukagua kumbukumbu zote za fedha na kutolewa maamuzi na wanakikundi wenyewe

xiii.            Kutathimini maendeleo ya kikundi

xiv.            Kupanga mipango mipya ya nwaka husika

 

4.1 KAMATI YA UTENDAJI

a.       Kamati ya urtendaji ya itakuwa na wajumbe tisa, mwenyekiti, katibu, muweka hazina na wajumbe sita

b.       Itakuwa ikiitana mara moja kwa wiki au mwezi kwa mujibu wa haja na makubaliano ya watendaji kwa ridhaa ya mkutano mkuu..

c.       Wajumbe wa kamati ya utendaji watakaa madarakani kwa muda wa mwaka mmoja na wanaweza wakagombea tena kama watakuwa tayari kufaanya hivyo.

d.      Kamati ya utendaji itakuwa na mamlaka ya kusimamia shughuli zote za kikundi zilizoamriwa na wanachama

e.       Kupokea maombi ya wanachama wanaotaka kujiunga

f.       Maombi ya wanachama yatajadiliwa na wanacham wote katika kikundi

g.      Kuhakikisha kuwa wakopaji wanarejesha madeni yao kama walivyoahidi na kuwachukulia hatua za kisheria wakopaji wasio waaminifu

h.      Wajibu mkuu wa kamati ya utendaji ni kusimamia utekelezaji, maazimio na maelekezo halali ya mkutano mkuu

i.        Kusimamia matumizi yote ya kikundi

j.        Kuandika na kutunza mihutasari ya majadiliano na maazimio yote ya mikutano ya kikundi

 

4.2 KAMATI YA NIDHAMU

Kamati ya nidhamu itashughulikia mambo yote ya kinidhamu ndani ya kundi.

a.       itachaguliwa na wajumbe katika mkutano mkuu

b.      itakuwa na wajumbe watatu

c.       itasuluhisha migogoro kwa kushirikiana na wanachama pale itakaposhindikana kwao

d.      itatoa adhabu kwa mwanakikundi kulingana na kosa lake.adhabu ambayo ni ya kujenga umoja na kushikamana

e.       itapendekeza adhabu za kutolewa kwa wajumumbe wakorofi ikiwa pamoja na afini

f.       itatoa taarifa ya kinidhamu ya mwaka katika mkutano mkuu

 

 

4.3 BODI YA WADHAMINI

kutakuwa na usimamizi wa bodi ya wadhamini yenye wajumbe waiopungua tisa ambao watachaguliwa na mkutano mkuu.

 

4.4. SIFA ZA WADHAMINI

            a. awe mwanachama hai wa USESCO FAMILY

            b. awe na umri usiopungua miaka 18 na kuendelea

            c. awe na akili tiamau

            d. awe mwaminifu kwa wanakikundi na jamii kwa ujumla

 

4.5  MAMLAKA YA BODI YA WADHAMINI

a.       watawachagua mwenyekiti na katibu miongoni mwao

b.      watasimamia na kutunza mali za DUSESCO FAMILY

c.       watasimamia na kuhakikisha akaunti ya kikundi imefunguliwa katika taasisi yoyote ya kifedha iliyosajiliwa kisheria

d.      watakuwa na jukumu la kutafuta misaada kutoka kwa wahisani wa ndani na nje ya nje ili kuchangia maendeleo ya  kikundi

e.       kukaimu kwa muda madaraka ya uongozi endapo tu utatolewa na wanakikundi au kujiuzulu. muda wa kukaimu usizidi siku tisini na ndani ya kipindi hicho uongozi utaitisha uchaguzi kuziba pengo hilo.

f.       bodi ya wadhamini itawajibika moja kwa moja kwa wanachama  wa DUSESCO FAMILY

 

5.0 VYANZO VYA MAPATO

i.                    ada ya kiingilio

ii.                  ada ya kila mwezi

iv.                michango ya wanachama

i.                    faini

ii.                  mfuko wa hisa

iii.                chakavu

 

5.1 MAKOSA YATAKAYOTOZWA FAINI

i.                    mwanachama atakayeongea ndani ya mkutano bila ya kuruhusiwa na uongozi au simu yake ikaita kwa mlio mkubwa na kusababisha kuharibu mazingira ya utulivu atatozwa faini ya shilingi 1000/= papo hapo

ii.                  mwanachama atakayechelewa kufika kwenye mkutano wa kikundi kama ilivyokubaliwa na wanachama wote bila taarifa atatozwa faini ya Tsh. 500/=

iii.                mwanachama atakayekosa kuhudhuria mkutano bila taarifa yoyote kwenye kikundi atatozwa faini ya Tsh. 2000/=

iv.                mwanachama atakayeshindwa kuhudhuria kikao cha kikundi kwa shughuli zake binafsi nje ya ruhusa za ugonjwa, kufiwa,au kuhitajika kazini atatakiwa kulipa faini ya shilingi 3000

 

 

WANACHAMA WAANZILISHI WA KIKUNDI

NA
JINA
CHEO
SIMU
SAINI
1
HAKIMU JUMA MLEMBELE
M/KITI
 
 
2
DEBORAH LYIMO
KATIBU
 
 
3
HILTRUDA AUGUSTINO
MHASIBU
 
 
4
PHILIP CHARLES KUBECHA
ADMIN
 
 
5
WINFRID MWANANENGULE
MWANAHABARI
 
 
6
SALMA DOLLAH
MJUMBE
 
 
7
ROSE MBWANA
MJUMBE
 
 
8
EDGER PETER
MJUMBE
 
 
9
EMANUEL MALUGU
MJUMBE
 
 
10
MISHY FIKRIN
MJUMBE
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni